Habari za kusikitisha kutoka kijiji na kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ni kwamba watu zaidi ya 20 wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa inayonyesha eneo hilo hadi hivi sasa.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo,mawe imenyesha usiku wa kuamkia leo na kuangusha nyumba na miti katika eneo hilo.

Hali hiyo inadaiwa kuleta majanga zaidi kutokana na nyumba zilizojengwa kwa udongo kuharibiwa vibaya na mvua hiyo kubwa.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema hali siyo shwari kwani nyumba nyingi zimeharibiwa vibaya,miti imeanguka na sasa miili ya marehemu na majeruhi inakimbizwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama. 

Dunia Kiganjani blog imeambiwa kuwa hadi sasa mvua bado inaendelea kunyesha ingawa siyo kubwa kama ile ya usiku na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka wilayani Kahama wamefika eneo la tukio.


Ally Tz blog inafuatilia tukio hili, na tutakuletea taarifa kamili hivi punde,endelea kutembelea Ally Tz blog.

Facebook Blogger Plugin by AllyTz

Post a Comment

 
Top