.
Ndoto ya mtoto wa TMK
ambaye aliwahi kusema hajutii kutokea kwenye familia ya kimasikini leo
ndoto yake ya kutembelea nchi mbalimbali duniani imetia, anatembelea
hizo nchi na analipwa.
Niliwahi
kuzungumza na Asley akaniambia kuna mengi bado hajayatimiza kwenye
maisha yake japokuwa kwa kiasi chake anaona mabadiliko toka ameanza
kufanya muziki, ni mtoto ambaye ametoka kwenye familia isiyo na uwezo wa
kifedha.
Kuna siku
niliwahi kwenda nyumbani kwa wazazi wake mwendo wa dakika kama 60 nje
ya mji wa Dar es Salaam, wazazi wake walifurahi sana na wakanichukua
mguu kwa mguu mpaka kwenye nyumba ambayo wakati huo Asley alikuwa
anawapa pesa kidogo kidogo waijenge, nilipokwenda kuiona ilikuwa
imefikia kwenye rent.
Kama
ulikuwa hajui pia muimbaji huyo kiongozi wa Yamoto Band, Asley aliwahi
kukasirishwa sana na kuumia moyoni kwa muda mrefu kwa kisa cha Baba
yake mzazi kufungwa polisi baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba
ambayo walikuwa wakiishi na ndio maana akajipanga mpaka kuwasaidia
wazazi wake na kumpa mama yake mzazi pesa ya mtaji.
Leo hii Asley anaendelea kupokea baraka za wazazi milango inafunguka na sasa yeye na Yamoto Band wameondoka Tanzania kwenya Uingereza.
Yamoto Band wakiwa wameshawasili nchini Uingereza.
‘Hii
ni mara yetu ya kwanza kwa Yamoto Band ndio tunaenda , tunamshuru
mwenyezi Mungu kwa hiyo itakuwa ni safari yetu ya kwanza huko tutakaa
wiki mbili, tuna show mbili lakini bado show moja hatuja confirm, show
ya kwanza itakuwa tarehe 21 na show ya pili itakuwa tarehe 22, kusema
kweli tuna vitu vingi vya kuzungumza unajua wengine ndio mara yetu ya
kwanza kwa hiyo vitu vingi tunakuwa na hamu navyo kama barabara zao,
magorofa na vitu vingi tu, asilimia 90 za sehemu tulizofanya show yaani
show zetu watu wanakubali vizuri lakini Arusha wanatuonesha maajabu sana
kwasababu sisi tunaamini kule ni Hip Hop halafu ukiingia kwenye show
unakuta watu wamejaa”–
.
Naye mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na
Wanae, Yamoto Band na Wanaume Family Said Fella akazungumza machache
kuhusiana na show ya Yamoto Band nchini Uingereza na kusema ;…‘
Niliwauliza
tu kwasababu siwezi kushangaa maana TMK wameshawahi kwenda na pia hata
Naseeb, kwa hiyo niliwauliza kwa Yamoto Band wanataka kwa CD au Live
wakaniambia kuwa wanataka muziki wa Live nikasema muziki tulioubuni ndio
huo sasa unatambulika sasa duniani, mpaka sasa mkataba wetu tuliofanya
na kampuni ya Zuri kwamba tumekubaliana yamoto watakuwa na show mbili
London’–alisema.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment