Tatizo la kukatika kwa umeme katika Jiji la Dar es Salaam litakwisha baada ya Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kutoa msaada wa zaidi ya Sh bilioni 66, kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo vipya vya kupozea umeme jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felchesmi Mramba
alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu
ya Tanesco Dar es Salaam.
Mramba
alisema mradi huo utakapokamilika utapunguza mzigo kwenye vituo vya
Oysterbay, Mbezi Beach na Makumbusho hivyo kuondoa adha ya kukatika kwa
umeme kutokana na kuzidiwa.
“Vile
vile wananchi wanaoishi maeneo jirani na vituo vipya watapata umeme wa
uhakika na ulio bora zaidi. Kituo cha kupozea umeme cha Ilala
kitaongezewa transfoma mbili hivyo kuweza kutoa umeme mwingi zaidi
kwenye maeneo ya katikati ya Jiji pamoja na Kariakoo,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa, Kituo cha Muhimbili kitakuwa na laini ya peke yake
itakayopeleka umeme kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo kuwa na
umeme wa uhakika.
Mramba
alisema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na ya Japan walikubaliana
kukarabati miundombinu ya umeme kwa kupanua na kujenga vituo vipya vya
kupozea umeme katika Jiji la Dar es Saalam.
Alitaja
kazi zitakazofanyika katika mradi huo kuwa ni ukarabati wa kituo cha
kupozea umeme cha Ilala kwa kuweka transfoma mpya mbili za ukubwa wa MVA
60,kV 132/33.
Vile
vile ujenzi wa jengo jipya la ‘control’ katika kituo cha kupoozea umeme
cha Ilala, uwekaji na uvutaji wa waya wa njia ya pili ya kusafirisha
umeme ya msongo wa kilovoti 132 kutoka Ubungo hadi Ilala na kupanua
kituo cha kupozea umeme cha Msasani 33/11kV kwa kuweka transfoma
nyingine mpya ya MVA 15, Kv 33/11.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment