WATU
wawili wamekufa mkoani Singida katika matukio tofauti yaliyotokea hivi
karibuni, likiwemo la mwanamke mmoja kupigwa na rungu na mumewe kutokana
na kile kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa
Polisi wa mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema kuwa tukio la kwanza
lililotokea kijiji cha Songambele, kata ya Ndago wilayani Iramba
Januari 11 mwaka huu majira ya saa 1.00 asubuhi ni la mauaji ya Maria
Shila (57) yaliyofanywa na mumewe Lucas Kitundu (47).
Akisimulia
mkasa huo, Sedoyeka alisema kuwa kabla ya tukio hilo wana ndoa hao
walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara ambapo Kitundu alikuwa akimtuhumu
mkewe Maria kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao.
Alisema kuwa
siku ya tukio, wanandoa hao walionekana klabu ya pombe ya kienyeji
wakiwa wanalumbana na asubuhi ya siku iliyofuata mwili wa Maria
uligundulika ukiwa umetelekezwa nje ya nyumba yao huku pembeni mwake
kukiwa na rungu lililojaa damu.
“Aliyegundua
mwili huo ni mdogo wa marehemu ambaye alikuwa na miadi ya kumpitia siku
hiyo kwa ajili ya kwenda naye kanisani,” alisema Kamanda Sedoyeka.
Kamanda Kamwela
alisema kuwa uchunguzi wa awali wa Polisi unaonesha kuwa Kitundu
alikuwa akiishi nyumbani kwa marehemu na mara baada ya kufanya kitendo
hicho alichukua vitu vyake, zikiwemo nguo, na kutoweka kusikojulikana
ambapo hadi sasa hajapatikana.
Katika tukio la
pili lililotokea Januari 12 mwaka huu huko katika kijiji cha
Mguluwang’ombe wilayani Manyoni, mtoto Laurent Buji (5) alipoteza maisha
akiwa njiani kupelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutumbukia
kwenye shimo la choo lililokuwa limejaa maji.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment