Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul
‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa
faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo,
Aunty Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi
karibuni, Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa
kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea
ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu
napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama
na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment