Pingu na Desso
Msanii wa zamani wa kundi la Tiptop Connection, Pingu amesema hana bifu yoyote na viongozi wa kundi hilo Abdu Bonge, Babu Tale wala Madee.
Msanii huyo amesema kama muziki ukiendelea kuwa mgumu ataomba msaada wao. “Mtoto anapokua anaanza kwa kukaa, kutambaa mwisho wa siku anasimamia kitu baadaye pekee yake na kuanza kutembea.”
“Mimi nilivyokuwa kule nilikuwa kama mtoto nayelelewa na kuishi katika mazingira ya maisha bora, kwahiyo sasa hivi naishi maisha ya mtaani nakomaa angalau niweze kujitegemea,” Pingu alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.

Katikati ya mwaka 2014, Pingu aliachia wimbo uitwao ‘Leo Leo’ aliyomshirikisha Nay wa Mitengo na Sheby Love lakini haUkufanya vizuri kama alivyotarajia.
“Unajua unavyokuwa chini ya usimamizi kuna mambo mengi mazuri unafanyiwa pamoja na kusimamiwa suala promo ya nyimbo, kusambaziwa katika vituo vya redio, kutengeneza video na kuandaliwa shows.
Lakini unavyokuwa peke yako kuna vitu unafeli lakini mambo yakiendelea hivi kusuasua nitarudi na kuwaomba waendelee kunisimamia ili malengo yangu yatimie.”
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment