
Katika
kukabilina na matukio ya mauaji na ukatwaji viungo vya watu wenye
Albinisim ambayo yameanza tena kushika kasi mwishoni mwa mwaka jana
serikali imepiga marufuku wapiga ramli ikiwa ni pamoja na kuunda kikosi
kazi kwa ajili ya operesheni maalum ya kuwasaka watuhumiwa.
Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mathias Chikawe ameyasema hayo jijini Dar
es Salaam ambapo amekiri kuongezeka kwa matukio hayo tangu mwishoni mwa
mwaka jana na kuongeza kuwa timu hiyo itaundwa na watu sita wawili
kutoka chama cha Albinisim Tanzania na wanne jeshi la polisi na wataanza
na mikoa mitano ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora na Geita na baadae
Sumbawanga, Kagera na Mbeya.
Akijibu
maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari likiwemo la malalamiko ya
ucheleweshwaji wa kesi pamoja na watuhumiwa kuachiwa bila kufikishwa
mahakamani Mh Chikawe amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kudai kuwa
linatokana na msongamano wa kesi zilizopo mahakamani na kuongeza kuwa
kwa sasa wameanza mkakati ya kuzipa kipaumbele kesi ambazo zinaigusa
jamii moja kwa moja.
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye Albinisim nchini Bw Ernest Kimaya amesema
katika kukabiliana na tatizo la ucheleweshwaji wa kesi pamoja na watu
wanaoachiwa huru kwa kisingizio cha kukosa ushahidi wa kutosha chama
hicho kinatafuta udhamini kutoka mataifa ya nje ili wapate fedha za
kuendesha kesi kwani hadi sasa kesi zilizofanyiwa kazi ni tano tu kati
ya kumi na moja.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment