Habari Bongomovies, Kwanza kabisa nawapongeza kwa kutupa
fursa na sisi mashabiki wenu kuweza kutoa yetu ya moyoni kuhusu
tasnia yenu ya filamu.
Kwanza kabisa mimi ni mshabiki namba moja kabisa wa “madame” (Wema
Sepetu) tangu akiwa Miss na alipoingia kwenye tasina ya filamu ndipo
nimezidi kumpenda zaidi, nimekuwa ni moja kati ya followers wake kwenye
mitandao yote ya kijamii na zaidi huwa sikosi ile show yake ya “In My
Shoes” nimeanza hiyo ili niweze kueleweka vizuri.
Swali langu kwa madame ni kwamba ile filamu ya “DAY AFTER DEATH”
(D.A.D) aliyomshirikisha muigizaji kutoka nchini Ghana, Van Vicker
inatoka lini?.
Kama kukumbukumbu zangu zipo vizuri , mwishoni mwa mwaka jana madame
alikwenda nchini Ghana nakukutana na mwigizaji Van Vicker ambako
walisema wanatengeneza filamu itakayo kwenda kwa jina la Day After Death
na kutuaidi kuwa itatoka muda sio mrefu.
Kitu ambacho nilifarijika nakumpongeza sana madame kwenye mitandao ,
sio kwasababu tu nampenda na kumkubali bali niliona amefanya jambo zuri
la kuvuka mipaka, sasa wasiwasi na mashaka yangu ni kwamba mbona hadi
leo hii kimya, hata kusikia kuwa itatoka lini?.
Tafadhari madame naomba utujuze, au tuamini kuwa ilikuwa ni PROJECTIIII tu?.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment