Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika
wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye umri wa
miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati
wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes.
Walioshuhudia
tukio hilo wamesema limetokea Februari 24 mwaka huu, saa 7 na nusu
mchana katika darasa la tano katika Shule ya Msingi Ilola iliyopo katika
Kata ya Ilola, Tarafa ya Itwangi, Wilaya ya Shinyanga.
Wamesema
mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu
za kichwani na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sophia Mathew (12).
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment