Mwanamziki na mwigizaji wa filamu za Bongo, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’, ameamua kuweka wazi chanzo cha migogoro yake na
mumewe mtarajiwa, Nuh Mziwanda kuwa ni marafiki.
Shilole alidai kuwa mara nyingi wamekuwa wakigombana, lakini chanzo
kikiwa ni maneno ya uchonganishi kutoka kwa marafiki zao wa karibu ambao
wana lengo la kuwatenganisha.
Mwanadada huyo alidai kutokana na hali hiyo, hivi sasa ameamua kutowahusisha suala lolote linalohusu maisha yake ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara baina yao.
Alisema wale walio karibu yao ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa
kutokea kwa migogoro kwenye mahusiano yao, ukizingatia hivi sasa wapo
kwenye harakati za kufunga ndoa baada ya wazazi wa pande zote kukubali
uhusiano wao.
“Tumegundua kuwa mashoga ndio wanaotugombanisha, kwani kila mara
mchumba wangu anapewa taarifa zinazonihusu mimi huku hao hao wakiniletea
habari zake, jambo hili limesabababisha nisihitaji tena marafiki wengi
wao ni wanafiki,”alisema.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment