Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia, Erick Bruno (30) kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mpenzi wake, Daja Dungu (35) wakati walipokuwa kwenye nyumba ya kulala wageni (jina tunalo) Manispaa ya Morogoro.
Akizungumzia
kutokea kwa tukio hlo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard
Paul, alisema tukio hilo lilitokea Februari 23, mwaka huu saa 6.30 usiku
katika karakana ya Kichangani ambapo mtuhumiwa alikodisha chumba namba
nane, akiwa na na mwanamke huyo.
“Februari
23, mwaka huu saa sita na nusu mtuhumiwa alifika kwenye nyumba hiyo
akiwa ameambatana na huyo mwanamke kwa lengo la kufanya ngono baada ya
muda kukasikika kelele za kuomba msaada,” alisema Paulo.
Paulo
alisema baada ya kelele hizo mlinzi wa nyumba hiyo aliwaita watu na
kumtaka mtuhumiwa afungue mlango, lakini alikataa kwa kudai kuwa hakuna
kitu kilichotokea, ndipo juhudi za kuufungua mlango zilifanyika na
kumkuta mwanamke huyo akiwa amefariki.
Aidha,
Paulo alisema Polisi bado haijafanikiwa kupata chanzo cha tukio hilo na
kuwa upelelezi unafanyika ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani
kujibu mashtaka yanayomkabili.
Kamanda Paul, alisema mtuhumiwa anashikiliwa Polisi kwa upelelezi zaidi na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment