Mwigizaji na muongozaji wa fiamu hapa Bongo, Jacob
Stephen ‘JB’ ameitaja filamu ya Mzee wa Swaga kua ndio bora zaidi kati
ya filamu zake zote tangu aanze kuigiza.
“Kosa la defence ...ni goli....nafasi ya 1.ndugu zangu. Tangu nianze kuigiza hii movie naipenda sanaaa....”-JB aliandika.
Wakati ya filamu ya Mzee wa Swaga ambayo imetoka mwanzoni mwa mwaka
huu akiitaja kuwa namba moja, namba mbili ilikwenda kwa filamu yake ya
14 Days, tatu, Senior Bachelor , nne, DJ Ben, huku tano akiitaja filamu ya Nakwenda kwa Mawanangu.
JB alizitaja tano zake bora ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa mashabiki wake mtandaoni siku chache zilizopita. SOMA HAPA
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment