Wikiendi iliyopita mastaa wa sinema za Kibongo, Jacob
Steven ‘JB’ alijikuta akiangua kilio na kuungwa mkono na mastaa wenzake,
Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ na Single Mtambalike ‘Richie’
walipomtembelea wodini mama mzazi wa mtoto Albino, Yohana Bahati (1)
aliyeuawa kikatili, Ester Thomas (30) ambaye naye alijeruhiwa vibaya
kichwani.
Tukio hilo la majonzi lilijiri kwenye Hospitali ya Bugando mkoani mwanza ambapo wasanii hao walikwenda kumfariji mama wa mtoto huyo
aliyetekwa mjini Geita hivi karibuni.
Walipofika wodini hapo, JB na wenzake walitoa yao ya moyoni kupinga
vikali ukatili aliotendewa mama huyo na mwanaye huku wakitahadharisha
juu ya laana inayoweza kuikumba jamii yetu kwa tukio hilo.
JB: Nampa pole sana mama Yohana. Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na jamii pana duniani.
Watu hawafanyi kazi kujipatia kipato halali. Mafisadi wanataka kujipatia fedha kupitia njia za kishetani za kuwaua wenzetu. Albino ni wenzetu na tunawapenda. Lazima wahalifu wakamatwe na wahukumiwe kunyongwa.

Richie: Natokwa na machozi. Hiki ni nini? Hatuwezi kufumbia macho jambo hili hasa sisi wenye nafasi kubwa ya kukemea vitendo hivi.
Mara baada ya mastaa hao kutoa la moyoni katika wodi aliyolazwa mama
huyo, iligeuka kama msiba kwani kila aliyekuwepo alikuwa akiangua kilio
kwa uchungu.
Tayari mtoto Bahati amezikwa baada ya mwili wake kupatikana ukiwa
hauna baadhi ya viungo huku mama yake akiendelea na matibabu baada ya
kufanyiwa oparesheni sehemu ya kichwani aliyojeruhiwa vibaya wakati
akinyang’anywa mwanaye.
Tunampa pole sana mama Yohana Bahati, watanzania tuungane kupinga ukatili huu.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment