Mwanamke mmoja ameieleza mahakama ya nchini Kenya kwamba alilazimika kumuuza mtoto wake wa siku tano kutokana na umaskini wa kupindukia ambao ulisababisha kukosa fedha za kumtunza mtoto huyo.

Mama wa mtoto huyo Virginia Mwangi aliiambia Mahakama ya Nyeri kwamba alilazimika kumuuza mtoto huyo Shilingi 7,000 kwa Eunice Wangeci Kibira ambaye pia alishtakiwa kwa kosa hilo.

Wanawake hao wawili wanakabiliwa na mashtaka manne ya kushirikiana katika biashara ya kumuuza mtoto huyo kinyume na sheria ya watoto.

Mwangi alikiri makosa hayo mbele ya mahakama hiyo lakini Wendi alikanusha mashtaka na kuachiwa kwa dhamana ya shilingi 50,000.

Facebook Blogger Plugin by AllyTz

Post a Comment

 
Top