Chanzo kililitonya Ijumaa kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, Chid aligoma kulipa gharama za matengenezo ya gari hilo hali iliyozua mzozo mkubwa.
“Chid alikuwa mtata sana kukubali kosa, mzozo ukawa mkubwa, watu wakajaa lakini baadaye wakamalizana na kila mmoja akaendelea na safari zake,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizi, paparazi wetu alimtafuta Chid kwa njia ya simu yake ya mkononi, alipopatikana alidai alikuwa katika kikao cha familia hasingeweza kuongelea suala hilo.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment