Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan amesema kuwa anatamani kupata
mtoto wa pili kwa sababu mtoto wake wa kwanza amefikisha miaka 10,
tatizo hana wa kuzaa naye.
Tiko Hassan
Akipiga stori na Ijumaa Tiko alisema yeye ni ‘mgonjwa’ wa watoto
wachanga na anahisi sasa ni muda muafaka ila tatizo mwanaume aliyenaye
hana mpango wa kupata mtoto.
“Yaani acha tu, mpenzi niliyenaye naona kama hajajiandaa maana hata
nikiongelea ishu ya kubeba mimba, naona ananipotezea lakini kiukweli
nahitaji mtoto wa pili,” alisema Tiko.
Facebook Blogger Plugin by
AllyTz
Post a Comment