Mbunge wa Mbinga Mh.
Kapten John Komba amefariki dunia leo saa kumi jioni katika hospitali ya TMJ
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtoto
wa marehem Jerry Komba,amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa
wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake
Mbezi Beach.
Katibu wa mbunge
Gasper Tumaini alisema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ na
ndipo mauti yalipomkuta.
Katibu huyo alisema
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hosp ya Lugalo jijini Dar Es salaam ambapo
ratiba ya maziko bado haijafahamika.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment