WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea jana asubuhi
kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na
kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye
oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la UPENDO.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment