Bwana Malick Bandawe amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa
tangu atengane na mzazi mwenziye, Rose Ndauka bado hajatokea wa
kumtetemesha.
Akimzungumzia Rose, Malick alisema kuwa huko nyuma alipomuona Rose
alimtetemesha na kuamua kuingia mzimamzima mpaka kufikia hatua ya kupata
naye mtoto lakini mpaka sasa hajatokea kama yeye.
“Unajua mambo yanapotokea lazima kukubaliana nayo na huwezi
kulazimisha. Tangu uhusiano wetu usambaratike, hajatokea kama Rose,”
alisema Malick.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment