Wakazi wa Ilula Mkoani Iringa wamegoma kupokea maiti ya mama aliyeuwawa wakati wa mapambano yalioyotokea juzi mkoani Iringa kati yao na polisi kwa masharti mawili:
 
Mosi: Wananchi 18  Waliokamatwa  na  jeshi la polisi  baada  ya vurugu  hizo  waachiwe  mara  moja  bila  masharti  yoyote.

Pili: Polisi walio sababisha mauaji hayo wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria .
Katika tukio hilo, wananchi wa Ilula walimtuhumu polisi kumuua mwanamke kwa kosa la kuuza pombe muda wa kazi na hivyo kupanda ghadhabu na kuvamia kituo cha polisi ambako walichoma magari matano madogo na basi moja na baadaye kwenda kufunga Barabara ya Dar es Salaam- Mbeya kwa muda wa saa tano hadi Jeshi la Polisi lilipoongeza askari wake kutuliza ghasia hizo

Facebook Blogger Plugin by AllyTz

Post a Comment

 
Top