Miongoni
mwa matukio ya kushangaza kama sio kufurahisha yaliyofanywa siku ya Jumamosi
Feb.14 katika siku ya wapendanao Valentine’s day, ni lile la wachumba kumi
walioamua kufunga ndoa zao wakiwa ndani ya jeneza huko Bangkok, Thailand.
Tukio
hilo ambalo lilikusanya mamia kwa maelufu ya ndgu na wageni waalikwa imekuwa
kali ya mwaka ambapo jeneza kubwa lilokuwa limepambwa kwa rangi ya pinki
lilowekewa mto mkubwa kisha maharusi kungia ndani na kulala chali kisha kila
mmoja kubeba ua.
Baada ya
kulala chali wazee wawili wa kimila waliovaa nguo za rangi ya Chungwa
wanawafunika na shuka nyeupe kisha nyimbo za kimila huimbwa na vigelegele
kuendelea kama kawaida.
Inasemekana
kuwa wapenzi hao walifanya hivyo kwa kuamini kuwa ni njia ya kuondoa mikosi
katika ndoa zao.
Wazee wa kimila wakiendelea na shughuli.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment