Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza
Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya
hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam
Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na
E.L. James.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua kwamba
haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini.
Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na
Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 kifungu cha 15 (i) na kifungu 18(i na ii) ambayo ufafanuzi wa
utekelezaji wake uko katika Kanununi za Sheria hiyo Kifungu cha 24
vifungu vidogo vya a,b,d,e,n na t.
Filamu ya FIFTY SHADES OF GREY hairuhusiwi kuonyeshwa popote
Tanzania.
Aidha, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania
inawakumbusha kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu Wamiliki wote wa kumbi
za sinema na maeneo yote ya kuonyeshea filamu kuwasilisha filamu katika
Bodi hiyo ili zikaguliwe na kupangiwa daraja kabla hazijaanza
kuonyeshwa na kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria.
Pia uzinduzi wowote wa filamu unaofanywa katika kumbi za sinema na
maeneo yoyote ya kuonyeshea filamu ni lazima uwe na kibali kutoka Bodi
ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment