Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya muungano umemalizika leo kwa bunge kujadili na kupitisha maazimio ya jinsi ya kumaliza migogoro ya ardhi nchini.
Katika
maazimio hayo yaliyopokelewa na serikali , serikali imeziagiza mamlaka
husika kuwachukulia hatua watendaji wote waliopewa dhamana za uongozi
ambao wanasababisha migogoro ya Ardhi, Wakulima na Wafugaji kuendelea na
kuifanya kama miradi yao ya kujiingizia kipato katika kufanya
usuluhishi.
Akipokea
mapendekezo ya kamati teule iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza na
kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi, kilimo, Mifugo,
Maji na Uwekezaji Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema Serikali
imepokea mapendekezo yote saba yaliyotolewa na kamati hiyo na kuahidi
kuyafanyia kazi.
Pinda
amesema kuwa Taarifa ya Kamati hiyo imeonesha kuwa migogoro mingi
imeshindwa kumalizika kutoka na baadhi ya watendaji kuifanya kama miradi
yao ya kiuchumi na kuendelewa kuyagawa makundi ya wakulima na wafugaji.
Katika
mkutano huo, jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya nyongeza
yameulizwa na kujibiwa na jumla ya maswali 15 ya msingi na 13 ya
nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa papo kwa papo kwa
Waziri Mkuu.
Mbali
na maswali hayo, bunge lilipokea na kujadili taarifa mbalimbali za
kisekta na zisizo za kisekta na kupitisha mapendekezo mbalimbali kwa
ajili ya kutekelezwa na serikali.
Mkutano huo wa 18 wa Bunge umehitimishwa leo, na Bunge kuahirishwa hadi Tarehe 17 Machi. 2015.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment