Jack: Sitaki Tena Ndoa!
Mrembo na mwigizaji wa filamu,
Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa
hayuko tayari kuolewa tena hii ni baada ya kupewa talaka na aliyekuwa
mumewe, Gadna Dibibi.
Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha
yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake.
“Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi
kusema ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike
kwanza sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena
upya,” alisema Jack.
Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa
talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment