
BAADA ya kukataa mara kwa mara juu ya uhusiano wao wa kimapenzi, hatimaye wasanii hao Jux na Vanessa Mdee juzi walikutwa katika mkao wa kimahaba kiasi cha kuwafanya mashabiki kujiuliza kama mkali huyo wa kibao cha Uzuri wako anaweza kuendelea kubisha.

Jux na Vanessa Mdee
Wawili hao walikutwa wamepakatana wakati wa onyesho la kutambulisha
video za wakali wa Bongo Fleva, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika
viwanja vya Escape One, Mikocheni jijini Dar.Vee Money alithibitisha kuwa wao ni wapenzi mbele ya umati alipokuwa stejini akiimba naye pamoja na Barnaba wimbo walioshirikiana unaojulikana kwa jina la Siri, akisema anampenda sana Jux na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment