Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, iliimarisha ulinzi wakati kesi ya ugaidi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake ilipotajwa.
Askari
walikuwa wengi katika eneo la Mahakama huku kila mtu aliyeingia getini
akikaguliwa kwa kifaa maalumu na kupapaswa ili kuangalia kama ana
silaha.
Jana kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda na kuahirishwa hadi Machi 4 mwaka huu itakapotajwa tena.
Wakili
wa Serikali, Peter Njike alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya
kutajwa lakini bado wanasubiri uamuzi wa rufaa waliyoikata katika
Mahakama ya Rufani.
Upande
wa Jamhuri ulikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, ulioamuru Mahakama ya Kisutu kusikiliza na kutolea uamuzi hoja
za washitakiwa.
Washitakiwa
wanadaiwa kati ya Januari mwaka juzi na Juni mwaka jana katika maeneo
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama ya kutenda kosa kwa
kutafuta watu wa kushiriki vitendo vya ugaidi.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment