Mwigizaji wa kike wa filamu Ligth butterfly Mushi ‘Light’
amefunguka kwa kusema kuwa hapendi kuigiza Komedi kwa sababu ni
udhalilishaji hasa kwa wanawake.
Anasema kuwa aliwahi kuchaguliwa
kucheza Komedi ya Inye lakini baadae aligundua kilichofanya achaguliwe
ni maumbile yake.
“Tunaigiza filamu hakuna udhalilishaji lakini kuna Komedi tuliwahi
kucheza ilikuwa inataka wasanii wa kike wawe na maumbile makubwa yaani
makalio, kuchesha makalio sasa huo si uchekeshaji ni udhalilishaji,
hicho ndio kilinifanya nichukie Komedi,”anasema Light.
Light anasema kuwa waandaaji wasiangalie tu maslahi yao tu pia
waangalie waigizaji nao maisha yao baadae wakiwa na familia zao na
wakiangalia filamu zao za Komedi zilizotolewa siku za nyuma watakuwa
katika hali gani, hali ambayo inamfanya asipende kuigiza Komedi
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment