mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa, Ijumaa Wikienda lina kitu kamili.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kwamba, tayari Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.
Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.
“Pia kuna dawa ambazo alipewa kwa ajili ya kumpatia nguvu zaidi,” alisema mmoja wa wanafamilia kwa ombi la kutotajwa gazetini.
Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa mama Diamond ambapo lilihakikishiwa kwamba bimkubwa huyo alikuwa ndani amelala na Diamond yupo nchini Afrika Kusini kikazi.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment