Odama Afunguka Kuchangia Wanaume!
Mrembo na wigizaji Jeniffer Kyaka ‘Odama’ amefunguka mengi kuhusiana na maswala ya mahusiano alipokuwa akifanyiwa mahojiaona na Ally Tz Blog.


Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo;
Paparazi: Mambo vipi Odama! Tuanze moja kwa moja na swali la kwanza, hivi kwa sasa una mpenzi? Mbona hatumjui?

Odama: Mambo poa! Mpenzi ninaye, nampenda muda bado wa kumuanika.
Paparazi: Ulishawahi kuchangia bwana na mwanamke mwingine katika maisha yako?
Odama: Hapana, sina kumbukumbu hiyo.

Paparazi: Hadi leo hii unaweza kukumbuka idadi ya wanaume ambao umewahi kutoka nao kimapenzi?Odama: Nakumbuka, kama mtu hukumbuki idadi basi lazima utakuwa una kichaa. Nakumbuka kwa sababu idadi ni ndogo, ila hapa sitataja idadi yao.

Paparazi: Hivi baba mtoto wako ni nani hasa au ndiye uliyenaye hadi sasa?
Odama: Hilo liweke kapuni kwa sasa, nitalizungumza ‘next time’.

Paparazi: Inasemekana wewe ni miongoni mwa warembo ambao wanaoongoza kwa kutongozwa Bongo Movies, ni kweli?

Odama: Hiyo kawaida kwa mtoto wa kike, nadhani sipo peke yangu.

Facebook Blogger Plugin by AllyTz

Post a Comment

 
Top