BAADHI ya vifaa vya abiria vilivyoporwa katika tukio la utekaji wa magari 11 uliofanywa na majambazi waliokuwa na silaha za jadi mkoani Manyara mwanzoni mwa wiki hii, vimekutwa vikizagaa katika maeneo yalikofanyika uporaji huo.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoani Manyara, Christopher Fuime alisema
vitu vilivyopatikana ni pamoja na laini za simu 14 na simu zinazouzwa
kwa bei ndogo na kwamba jeshi hilo linaendelea kuwasaka majambazi hao
ili kuwachukulia hatua.
Kamanda
Fuime alisema katika tukio hilo majambazi zaidi ya wanane wakiwa na
silaha za jadi waliteka magari 11 katika kijiji cha Gehandu kilichopo
katika barabara kuu ya Babati–Singida na kupora vitu mbalimbali kwa watu
waliokuwa ndani ya magari hayo zikiwemo fedha taslimu na simu za
mkononi.
Alifafanua
kuwa katika tukio hilo kiwango cha juu cha fedha zilizoporwa ni Sh
600,000 na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa kuwa majambazi hao
walipoona idadi ya magari yanazidi kuongezeka na kufikia 18 katika eneo
walipoweka vizuizi waliamua kukimbia kusikojulikana.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment