Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wafungwa wote wanaotumikia
kifungo chini ya miezi sita na mahabusu wanawapatia haki yao ya msingi
ya kupiga kura.
Akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje aliyehoji kuhusu
wafungwa kutoruhusiwa kupiga kura,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera, Uratibu na Bunge, Jenister Mhagama alisema kwa mujibu wa
ibara ya 5(2) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wafungwa
wote wenye vifungo chini ya miezi sita wanaruhusia kupiga kura.
Aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshaanza kufanya utafiti
pamoja na mazungumzo kupitia taasisi mbalimbali zinazohusika na wafungwa
kuweka utaratibu wa kuwawezesha kujiandikisha katika daftari la kudumu
la wapiga kura.
‘Wafungwa wanaotumikia vifungo vyao chini ya miezi sita wana haki ya
kupiga kura ya kuchagua viongozi wao na hiyo imeainishwa katika katiba
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema Waziri Mhagama.
Aidha aliongeza kuwa kwa wale wanaotumikia vifungo zaidi ya miezi sita
Serikali itangalia namna ya kuwasidia kwa kuzingatia sheria na kanuni
zinavyosema na kama katiba hairusu basi hawataweza kushiriki kupiga
kura.
Naye Mbunge wa Viti Maalum Maryam Msabaha alihoji kuhusu mpango wa
Serikali katika kuwapatia ajira wafungwa walioweza kuhitimu taalum
mbalimbali waliokuwa wakitumikia vifungo, ambapo Waziri Mhagama
alifafanua kuwa wafuate taratibu na sheria za kuomba ajira.
“Kwa upande wa wale wafungwa wanaohitimu mafunzo mbalimbali yanayotolewa
gerezani kabla ya kupata ajira ni vyema wakapata ushauri na baadaye
kuajiriwa au kujiajiri wenyewe ” alisema Mhagama.
Hata hivyo alisisitiza kwamba wafungwa wanapomaliza vifungo vyao huwa
watu huru wenye maamuzi yao binafsi katika kuendeleza maisha yao ya kila
siku katika kujiletea maendeleo yao.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment