Uchaguzi (NEC) imekabidhiwa jukumu la kuangalia
utaratibu utakaotumika kuwezesha Watanzania walio nje ya nchi kushiriki
kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika Oktoba mwaka huu.
Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akijibu
swali la Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF) aliyetaka kufahamu
maandalizi yaliyopo kwa ajili ya kuwezesha Watanzania waliojiandikisha
walio nje ya nchi , kupiga kura.
Mnyaa katika swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu kuwa Tanzania
ilisifiwa kukuza demokrasia kupitia Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la
Katiba aliporuhusu wabunge kupiga kura wakiwa nje ya nchi.
“ Kwa kuwa tuna uchaguzi wa Rais na Wabunge, na jambo hili linakwenda
vizuri, je utaratibu gani au maandalizi gani yamefanyika ili Watanzania
walioko nje ya nchi waliojiandisha waruhusiwe kupiga kura,” alisema
Mnyaa.
Waziri Mkuu katika majibu, alisema ingawa Serikali ilishajaribu
utaratibu huo siku zilizopita ikaonekana kuwapo matatizo ya kitaalamu,
jambo hili limepelekwa NEC waone ni utaratibu gani utatumika kuwezesha
walio nje ya nchi katika sehemu mbalimbali waweze kushiriki.
Alisisitiza kwamba anaamini Tume ya Uchaguzi itaona utaratibu mzuri ambao hautaleta kikwazo.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment