ALIYEMPONZA CHEKA HUYU HAPA

Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga ngumi na kumuumiza meneja wake
huyo, wakati alipokwenda kwa ajili ya kufuata fedha za mauzo ya baa yake
hiyo lakini wakapishana maneno yaliyosababisha tukio hilo lililowashtua
watu wengi.
Licha ya mashabiki wa bondia huyo aliyemaliza enzi za Snake Boy,
Rashid Matumla, watu wengine wanaodaiwa kumpa hofu Baraka ni pamoja na
wakusanya chupa za plastiki ambao walimtegemea Cheka kwa ajili ya kwenda
kuziuza katika kiwanda chake kilichopo maeneo ya Kihonda mjini hapa.
...Akipanda gari kwenda jela.
“Ukweli maisha ya huyu jamaa hapa Morogoro ni magumu sana kwa sababu
kila anakokwenda anakutana na watu wanaomnanga juu ya kitendo
alichokifanya. Watu wanaomtakia mema wanamshauri kuwa mwangalifu sana wa
nyendo zake kwani watu wanaweza kumfanya lolote maana Cheka ni mtu
muhimu sana hapa,” alisema shuhuda mmoja.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment