MKAZI wa mtaa wa Migongo kata ya Migongo Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, Hajili Mpili (52) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Masasi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.
Mtuhumiwa
alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki na kusomewa shitaka na
mwendesha mashtaka Suleimani Omari mbele ya hakimu Halfani Ulaya.
Mbele
ya Hakimu Halfani Ulaya, Mwendesha Mashtaka Suleimani Omari alidai kuwa
mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto wake Februari 5
mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake huko katika mtaa
wa Migongo.
Alidai
kuwa mshtakiwa alimlawiti mtoto wake aliyekuwa anaishi naye nyumbani
hapo baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia miaka mitatu iliyopita
na kwamba tangu hapo mzee huyo hajawahi kuoa tena.
Suleimani
alidai kuwa mtuhumiwa huyo kwa nyakati tofauti amekuwa akimlawiti mtoto
huyo huku akimpa vitisho vya kwamba endapo angethubutu kutoa taarifa
hizo kwa majirani, basi angeweza kuondoa maisha yake ili aweze kuepukana
na aibu hiyo.
Alisema
siku ya tukio mtuhumiwa huyo alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na
ndipo alipomvamia mtoto huyo na kuanza kumlawiti na ndipo mtoto huyo
alianza kupiga makelele ya kuomba msaada lakini kwa bahati mbaya hakuna
jirani hata mmoja aliyeweza kusikia sauti za mtoto huyo na alifanikiwa
kukimbia na kulala vichakani.
Mwendesha
mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa asubuhi mtoto huyo
alikuwa ameumizwa usoni pamoja na mgongoni kutokana na kipigo alichokuwa
amekipata usiku na kwamba alipoulizwa na watoto wenzake kwa nini ana
majeraha aliwaeleza amepigwa usiku na baba yake alipokuwa akijaribu
kujiokoa wakati akimlawiti.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment