Wizara ya Kazi na Ajira iko katika mchakato wa kuandaa Sheria mpya ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni ili kudhibiti kuajiriwa kwa wageni ili kufanya kazi ambazo Watanzania wenyewe wanaweza kuzifanya.
Alisema
mchakato huo uko karibu kukamilika na utapelekwa bungeni kutokana na
ratiba na kueleza kuwa itasaidia kudhibiti wafanyakazi wageni wanaoingia
nchini bila utaratibu maalum na kusababisha kuajiliwa kwenye kazi
ambazo wenyeji wanaweza kufanya.
Waziri
katika wizara hiyo, Gaudentia Kabaka aliliambia Bunge kuwa sheria hiyo
itatoa mwongozo juu ya utoaji vibali, kwani sasa kumekuwa na sehemu
nyingi hivyo kuwa na sehemu moja pamoja na adhabu kwa wageni wanaofanya
kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.
Alisema
hivi karibuni walibaini wageni 300 walioingia nchini kufanya kazi
katika kiwanda cha saruji cha Dangote, Mtwara kwa kazi zinazoweza
kufanywa na watanzania.
Wakati
huo huo, wafanyakazi zaidi ya 350 wa Kampuni ya mgodi wa Bulyanhulu
waliodai kuachishwa kazi baada ya kupata madhara wakiwa kazini
wametakiwa kwenda kwenye Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi
(OSHA) kupimwa ili kuthibitisha iwapo walipata madhara hayo kutokana na
kazi walizokuwa wakifanya ili kuweza kutibiwa.
Alisema
kuwa OSHA ndiyo wenye mamlaka ya kuthibitisha kuwa wafanyakazi hao
wameathirika na kwa utaratibu walitakiwa kupeleka OSHA barua kutoka kwa
mwajiri ili kuweza kupimwa na kujua athari walizopata wakiwa kazini
lakini tangu wafukuzwe kazi mwaka 2007 hawakupeleka barua hiyo.
Pia
alitaka chama cha wafanyakazi migodini (TAMICO) kuwaunganisha
wafanyakazi hao ili kufuatilia kwa pamoja na kuepusha kuwa mmoja mmoja.
Mbunge
wa Kisarawe, Suleiman Jafo (CCM) alisema wafanyakazi hao wamekuwa
wakihangaika katika ofisi mbalimbali ikiwemo kwenye Wizara ya Kazi na
Ajira kufuatilia suala hilo.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment