STAA wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefungukia mambo yake ya chumbani na kuanika kuwa anapenda kuvaa kufuli zenye rangi tofauti.

Batuli ambaye anaendelea kufanya vizuri Bongo Movies kila kukicha, alisema kama binadamu wengine na yeye linapofika suala la viwalo hivyo vya ndani, anapenda kununua vingi vyenye rangi tofauti.
 

 
Mwandishi: Mpenzi wako anapotoka kazini na kuja kwako huwa unapenda kumfanyia nini?
Batuli: Nina utundu wangu kama mwanamke, ila ni siri yangu.
 
Mwandishi: Nyakati za usiku unapokuwa nyumbani muda wa kwenda kulala, unapenda kumpigia simu nani kama mtu wa mwisho?
Batuli: Kwanza mpenzi wangu anapokuwa hayupo, wazazi wangu na watoto wangu wawili walioko shule.
 
Mwandishi: Hebu tuambie nini siri ya urembo wako?
Batuli: Ni kujizuia sana na ulevi, lakini pia huwa nakuwa makini na mwili wangu, mpenzi wangu pia anachangia urembo wangu pamoja na kujipangia ratiba nzuri ya chakula maana si kila chakula naweza kula.
 
Mwandishi: Ulishawahi kutoa mimba?
Batuli: Sijawahi na sitaki ila nina watoto wawili nawapenda sana.

Facebook Blogger Plugin by AllyTz

Post a Comment

 
Top