MKUU wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Betty Mkwasa amepiga marufuku shughuli zote za waganga wa kutoa uchawi maarufu kama lambalamba.
Alisema
sasa itaandaliwa amri halali na akisikia kijiji kina lambalamba, mtu wa
kwanza kukamatwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji kwani inaonesha
waganga hao wamekuwa na ushirikiano na viongozi hao.
Alitoa
kauli hiyo juzi baada ya kutembelea kijiji cha Uhelela na kukuta
lambalamba wamepiga kambi katika kijiji hicho baada ya wananchi kuchanga
fedha za kuwaita waganga hao.
Alisema
wananchi wamekuwa mstari wa mbele kubariki kazi za waganga hao jambo
ambalo linakuwa ni gumu katika kuwadhibiti na kuwabaini wachukuliwe
hatua.
Alisema
haoni sababu ya wananchi kuita waganga hao ilhali walishapigwa marufuku
katika wilaya hiyo na mkoa wa Dodoma kwa ujumla kwani wamekuwa wakiibia
wananchi kwa lengo la kutoa uchawi na kufanya wananchi kuendelea kuwa
masikini.
Pia
aliwaagiza watendaji wa vijiji kuwabaini watu wote wanaotumia waganga
hao na kukamatwa kwa waganga wote wanaofanya shughuli hizo. Alisema
ushirikina umekuwa ukirudisha nyuma wananchi kiuchumi.
“Uhelela
wamekaribisha lambalamba lakini ni kijiji ambacho kipo nyuma katika
suala la ujenzi wa maabara na wamekuwa wakichangia hadi Sh 50,000 kwa
kaya kuita lambalamba lakini ukiwaambia mchango wa maabara wamekuwa
hawatoi,” alisema.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment