
Meneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Babu Tale alisema hawawezi kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili
kupata fedha, hivyo hawajapewa kitu chochote.
Alisema Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote
atakayetangazwa kuiwakilisha CCM katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Meneja huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa
taarifa ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia
kampeni Lowassa.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz