MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA).
Kuna
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuelezea kwamba
kutakuwa na mgomo wa wafanya biashara wa mafuta nchini, na kwa hiyo
kutakuwa na uhaba wa mafuta ya jamii ya petroli.
Aidha, taarifa hizo zinawachochea watumiaji wa bidhaa hizo kununua kwa wingi ili kuepuka usumbufu.
EWURA
inapenda kuutaarifu umma kwamba taarifa hizo si za kweli, hakuna mgomo
wala tatizo lolote linaloweza kuhatarisha upatikanaji wa mafuta nchini,
na kwamba nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta, na hakuna haja ya wadau
kuwa na wasi wasi.
Umma
unakumbushwa pia kuzipuuza taarifa za namna hiyo kwa sababu ni za
upotoshaji na zinalenga kuvuruga hali ya utulivu wa soko la mafuta
nchini. Ikumbukwe pia kwamba ni EWURA tu yenye mamlaka ya kisheria ya
kuutaarifu umma juu ya hali ya soko la mafuta na upatikanaji wa bidhaa
zake.
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano, EWURA.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment