Mwigizaji wa filamu ambae ameingia kwenye bongo fleva,
Flora Mvungi ‘H.Mama’ amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa bongo
movie hawapendani ndio maana wanashindwa kufika mbali kisanaa.
Akinukuliwa na Gazeti moja la burudani, Flora alisema “Tukitaka
kufanikiwa lazima sote letu liwe moja ili tufanye kitu kizuri,siku zote
umoja ni nguvu cha msingi tukiamua kufanya kazi tusiangalie huyu bado
msanii chipukizi siwezi kufanya naye kazi wote tushirikiane ili tufanye
vitu bora na kupige hatua”.
Aliendelea kusema kuwa wasanii ambao tayari wamesha kuwa mastaa
wakitafutwa ili afanye naye kazi lazima atataka malipo makubwa na
ukiangalia bado chipukizi basi ndio mwanzo wa kakata tamaa.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment