Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana waliomaliza katika jeshi hilo, kutambua kuwa walikula kiapo cha utii wakati wa kuhitimu mafunzo, hivyo suala la kuandamana ni kinyume na kiapo chao.
Vijana
hao waliotumikia Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni za nyuma na kumaliza
mkataba wa miaka miwili, wameambiwa shinikizo lao la kulazimisha ajira
kwa kuandamana ni kinyume cha sheria za nchi.
Taarifa
kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Makao Makuu ya jeshi hilo,
jijini Dar es Salaam jana, ilisema kipengele kimoja cha masharti ya
kujiunga na JKT kinasema baada ya mkataba, wanapaswa kurejea nyumbani na
hawapaswi kudai jeshi liwatafutie ajira.
Ilieleza
kwamba masharti ya jeshi hilo, huwekwa bayana kwa vijana wanapojiunga
na JKT. Vijana hao wanatakiwa kujua masharti hayo na taratibu za JKT
na kuelewa kuwa JKT halitoi ajira.
Taarifa hiyo ilinukuu kipengele kimojawapo cha masharti, kinachosema
“Kwa kipindi chote nitakachokuwa ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa
nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na
baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga
Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi”.
Ufafanuzi
huo ulitolewa, kutokana na vijana zaidi ya 200 waliohitimu mafunzo ya
JKT kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2013, kutangaza hivi karibuni kuwa
wataandamana wiki ijayo kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete, kumweleza shida
zao, ikiwemo kutokuwa na ajira tangu wamalize mafunzo.
Jeshi
hilo lilisema ni vema vijana hao, wakatambua kuwa tatizo la ajira siyo
kwao peke yao, ni tatizo la ulimwengu mzima Tanzania, ikiwemo hivyo
wanashauriwa kutumia stadi za kazi kujiajiri wenyewe.
“Kutokana
na dhumuni la kuundwa JKT Taifa, halina dhamana ya kuajiri bali
kufunza vijana wa taifa hili umoja, stadi za kazi na uzalendo baada ya
hapo wawe wenye sifa za kuajiriwa hupata ajira katika taasisi mbalimbali
za serikari na binafsi,” ilisema taarifa hiyo.
Hata
hivyo, jeshi hilo limesema tangu mwaka 2003 hadi 2014, vijana 24,708
wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama. Kati ya hao, vijana
21,977 wakiwemo wavulana 17,307 na wasichana 4,670, wameajiriwa na
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kwa
upande wa Polisi, vijana 3,965 wameajiriwa ambao kati yao, wavulana
ni 2,943; Magereza wameajiriwa 2,139 kati yao wavulana ni 2,044;
Zimamoto vijana 100 wavulana wakiwa 78 na taasisi zingine wameajiriwa
vijana 592
Aidha,
alisema vijana 1,622 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali kamavile
migodi ya dhahabu ya Geita, Mamlaka ya Bandari na Shirika la Hifadhi la
Taifa (Tanapa).
Taarifa
hiyo ilisema JKT ilianzishwa Julai 10, 1963 kwa lengo la kuwaweka
pamoja vijana na kuwapa malezi, kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa
dalili za matabaka, zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.
Serikali ilirejesha mafunzo ya jeshi hilo kwa vijana wa kujitolea mwaka 2001 baada ya kusitishwa mwaka 1994.
Alisema
masharti ya kujiunga na jeshi hilo kwa vijana wa kujitolea ni
kuhakikisha wahusika wanafahamu masharti na taratibu, ikiwemo kuelewa
kwamba JKT haitoi ajira.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment