MWIGIZAJI na muongozaji wa filamu Bongo Luckey Luckamo
amewashukia wasanii wakubwa kuwa uwezo wao wa kuigiza ni mdogo sana
lakini baadhi ya watayarishaji wanawapenda kwa sababu ya mavazi yao
katika filamu kitu kinachosaidia kupunguza gharama kwao lakini kiwango
chao ni kidogo sana.
“Katika tasnia ya filamu kuna changamoto nyingi, lakini ngumu kuliko
yote ukikutana na filamu inayoshirikisha wasanii Nyota, tatizo kwani
wengi wao uwezo wao upo chini sana, lakini wanabebwa na mavazi tu kwa
sababu wapo nadhifu,”anasema Luckey.
Msanii huyo anasema kuwa kama si watayarishaji kutawaliwa na mawazo
ya kuamini kuwa wasanii wakubwa ndio wanaouza basi wasanii wakubwa
wangekuwa wamepotea na soko la filamu kutawaliwa na wasanii wenyewe
uwezo na si majina kama ilivyo sasa, ambapo wasanii wazuri hawapewi
nafasi.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment