Kufungwa kwa ofisi ya aliyekuwa
msanii nyota wa filamu marehemu Steven Kanumba ya Kanumba The Great,
mama mzazi Flora Mtegoa amegeuka mbogo baada ya kuulizwa kuhusu hatima
ya kikazi ya taasisi hiyo.
Watu wamezidi kunifuatilia mambo yangu, sitaki kabisa nimechoka, hii
kampuni haimhusu mtu yeyote, hili ni jambo langu siyo lazima niliweke
wazi, kama kampuni imekufa au itaendelea haiwahusu, wanaoamini imekufa
waamini hivyo, maana hata Yesu walisema atarudi hadi leo mbona
hajarudi? aliuliza kwa hasira mama huyo.
Ofisi ya mkali huyo wa filamu za Kibongo, aliyefariki ghafla miaka
mitatu iliyopita, ilikuwa eneo la Sinza Mori na ilifungwa wiki mbili
zilizopita, baada ya mama huyo kudaiwa kushindwa kumudu kodi mpya ya
pango ambayo ilipandishwa.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment