Mama mzazi wa Nay wa Mitego anahisi mwanae ni mfuasi wa jamii ya siri ya freemason na ameanza kusita kupokea fedha kutoka kwake.
Kwa mujibu wa mama yake, mafanikio ya haraka ya Nay yakiwemo kujenga
nyumba ya kifahari, kumiliki magari kadhaa na maisha yake ya kimilionea,
vimemfanya aamini maneno yanayosemwa na watu au kuandikwa kwenye
magazeti ya udaku kuwa mwanae amepata utajiri huo kwa njia isiyo halali.
“Kuna kipindi ambapo nimetoa wimbo wa Mr Nay baada ya kutoka ile
video nakumbuka mimi mama yangu huwa nampelekeaga hela ya matumizi kila
baada ya wiki mbili au mwezi mmoja. Kuna kipindi nilimpelekea hela
akasema ‘no’ mbona mimi hela bado ninayo,”
Nay anasema alimpelekea mama yake kiasi cha shilingi laki mbili ama
tatu na akagundua kuwa mama yake hasemi ukweli na kuna kitu kilikuwa
kikimsumbua akilini.
“Baada ya hapo akaniambia ‘kuna habari nasikia kuhusu huu wimbo wako
huu nimeona mambo ya ajabu ajabu mule nimeona magazeti majirani wamekuja
wameniambia hivi na hivi’,” aliongeza Nay.
“Halafu bahati nzuri nilikuwa nimetoka kununua hii gari yangu ambayo
natembelea sasa hivi ‘Morano’ alivyoniuliza hivyo nikaona mama yangu
hataki hela yangu sababu ana wasiwasi na hiki ambacho watu wanaongea.
Hilo ni tatizo lililonipa wasiwasi na moyo wangu ukaingia unyonge, for
real kabisa nikawa mpole.
“Lakini nikawa na imani kwamba endapo mama yangu angekuwa anatambua
kwamba huu muziki ungekuja kuniweka sehemu uflani tangu zamani angekuwa
ananisupport zile hustle mazingira magumu niliyokuwa napitia angekuwa
anajua basi sasa hivi ningekuwa naenda naye sawa.”
Nay amesisitiza kuwa mali anazopata ni neema za Mungu tu.
“Mwenyezi Mungu tu ameamua kuninyooshea kuniwekea mambo yangu sawa
japokuwa bado sijafika pale ninapotaka kufika,” alisisitiza rapper huyo.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment