
James Robertson akitembea maili 21 kwenda na kurudi kazini

James Robertson akielekea kupanda gari lake alilopewa bure aina ya Ford Taurus ambayo ndio iliyokua chaguo lake

James Robertson akitoa machozi ya furaha baada ya kuzawadiwa gari.
James Robertson mkaazi wa Detroit aliyetembea maili 21 kwenda kazini kwa
takribani muongo mmoja hatimaye apata gari baada habari zake kuenea
kwenye mitandao.
James Robertson ambaye amekua akitembea kwa miguu maili 21 kila siku
aliitwa kwenye kampuni inayouza magari na kupewa gari aina ya ford
Taurus iliiyokua ndoto yake ya rangi nyekundu na ndani ikiwa nyeusi na
sababu za yeye kuchagua gari aina hiyo alisema ni hua haina muonekano
mzuri nje lakini ndani ni imara ni aina ya gari inayofanana na uimara
wangu.
Alipoulizwa kama anaitaka yeye alijibu nimeipenda, mpaka sasa wasamalia
wema wameisha mchangia dola laki tatu kwa ajili ya kumsaidia James
Robertson aliyetembea umbali wa maili 21 kwenda kazini iwe jua iwe
theluji kwa takriban muongo mmoja sasa amekwamuliwa na wananchi
waliosikia historia yake na wauuza magari wengi walimwita kumpa gari
lakini aina ya gari aliyokua ndoto yake ni ford Taurus nyekundu huku
ndani ikiwa nyeusi.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment