Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Chanzo cha
kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo Daz
Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia dozi
ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar.
“Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua
kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho
ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi
wetu alimtafuta Ray C, alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz
ila akaomba asizungumzie walipofikia kwa sasa.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment