Mbunge
wa Vunjo Dkt Augustine Mrema (TLP) ametoa shutuma zake bungeni Dodoma
akimtuhumu mbunge wa kuteuliwa na rais James Mbatia kuwa amekuwa
akimpakazia mambo mabaya kwa wapiga kura wa jimbo lake kuwa ana UKIMWI
Mrema
amesema kuwa mbunge huyo amekuwa akipita jimboni kwa kwake na kusema
kuwa wasimchague mbunge huyo kwa kuwa ana UKIMWI na hana maisha marefu
hapa duniani
Ametoa
kauli hiyo bungeni Dodoma na kusema "Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge
halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo, na natangaza kuwa
nitagombea tena na hafi mtu hapa"
Amesema ataendelea na shughuli zake jimboni mwake kama kawaida kwa kuwa yupo imara kiafya
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment