
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeiagiza klabu ya simba kumlipa
beki wake wa zamani Donald Mosoti jumla ya fedha taslimu dola elfu kumi
na nne na mia nne ambazo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya
shilingi milioni 26,000,000/= ikiwa ni fidia ya kuvunja mkataba wake
kinyume cha sheria .
Kwa mujibu wa taarifa zilizoko, klabu hiyo imetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 baada ya shirikisho hilo kukubaliana na madai yake ya kuvunjiwa mkataba kinyume cha sheria .

Mosoti akiwa anajiandaa kumzuia mshambuliaji wa Azam Fc Kipre Thctche wakati akiwa anaitumikia Simba .
Katika barua iliyoripotiwa kutumwa kwa klabu hiyo kupitia ofisi za
shirikisho la soka nchini TFF endapo Simba itashindwa kulipa fedha hizo
ndani ya muda ulioshauriwa suala hili litafikishwa kwenye kamati ya
nidhamu ya Fifa kwa hatua zaidi .
Simba iliamua kuachana na beki huyu iliyemsajili toka kwenye klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika ya msimu uliopita huku beki huyo akilalamika mkataba wake kuvunjwa bila taratibu kufuatwa .
Beki huyo kwa sasa anachezea klabu ya Tusker ya nchini Kenya baada ya
kusajiliwa akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment