Polisi wakiwa kwenye mapigano na wahalifu hao.
IMEBAINIKA! Mapambano
na wahalifu wanaosadikiwa ni magaidi kwenye Kitongoji cha Amboni jijini
Tanga, yameingia sura nyingine baada ya wakazi wa kitongoji hicho
kuvujisha siri tano, Amani limenyetishiwa.
WALIKUWA NA WAPENZI
Kwa
mujibu wa mkazi mmoja wa eneo hilo, wahalifu hao walishakuwa na
wanawake kwenye eneo hilo, hivyo kama walikuwa na mpango wa kujua siri
za Jiji la Tanga ilikuwa rahisi sana.“Wale watu baadhi yao walikuwa na
wanawake hapa Amboni. Na hilo limebainika baada ya kutokea kwa mapambano
na wao kukimbia kwani na mmoja wao aliyekuwa na mwanamke hapa
hajaonekana tena,” alisema mtoa habari huyo.
WALIKUWA WAKICHENJI DOLA KILA BAADA YA SIKU MBILI
Habari
kutoka kwa mkazi mwingine zilidai kuwa, baadhi ya wahalifu hao walikuwa
wakienda mjini Tanga kila mara kwa shida ya kuchenji dola za
Kimarekani.“Kuna wakati nilikutana na watu wakisema wanatafuta maduka ya
kuchenji dola za Marekani, wakakosa na kwenda mjini. Nikawa nawaona
mara kwa mara tena wakienda mjini, nadhani ni kila baada ya siku mbili.
“Lakini sikujua wanapoishi wala kazi zao. Naamini ni haohao maana baada
ya mapambano na wao sijawaona tena tangu Ijumaa iliyopita,” alisema
mkazi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hans.
TABIA ZAO
Mjumbe
wa nyumba kumi wa kitongoji hicho, Idd Suleiman akizungumza na Amani
alisema kuwa, kulikuwa na watu walioonesha dalili kwamba si wenyeji wa
eneo la Amboni.“Mbaya zaidi, watu hawa walikuwa na tabia ya kuonekana
nyakati za usiku, kama ni mchana basi si kwa uwazi mkubwa. Nilijaribu
kuwafuatilia nikidhani ni wakazi wa mtaani kwangu lakini sikuwahi
kuwajua,” alisema mjumbe huyo.
WENGI WAO NI WAREFU, WEMBAMBA, WEUSI
Mjumbe
huyo alizidi kusema kuwa, watu hao waliokuwa wakionekana maeneo hayo ni
wembamba, wengine ni warefu na weusi lakini walionekana wakakamavu muda
wote.
“Kusema
kweli kama sisi wananchi tungekuwa watafiti sana na kutoa taarifa
polisi labda wangekamatwa mapema kwani watu hao walikuwa hawafanani na
sisi wakazi wa eneo hili ambao tunajuana,” alisema.
NI KWELI WAMEKIMBILIA KENYA?
Naye
mzee Juma Kabari ‘Mapipa’ yeye alisema kuwa, anavyojua miaka ya nyuma
kuna Mzungu aliwahi kumpoteza mbwa wake ndani ya mapango hayo.“Sasa
katika kumtafuta hakumpata, baadaye akaja kuonekana Mombasa nchini
Kenya. Ikagundulika kuwa, kuna pango moja ambalo linatokea Mombasa. Nina
wasiwasi kwamba, hata hawa jamaa (wahalifu), huenda walipita chini kwa
chini wametokea Mombasa, ndiyo maana hawajawakamata.
“Watu waliodaiwa kukamatwa juzi, siamini kama kweli ni miongoni mwa wale
ambao walitoa upinzani kwa askari wetu Ijumaa iliyopita,” alisema mzee
Mapipa.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment