Msanii wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’,
amesema anashangazwa na uvumi unaoendelea kuwa yupo katika uhusiano na
mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu.
Akielezea kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandano ya kijamii, Ommy
Dimpoz, alisema walikuwa Afrika Kusini kwa mapumziko ndipo picha hizo
zilipopigwa.
“Tunapiga picha nyingi sana na Wema hata uki-google utaziona, hii
siyo mara ya kwanza, lakini sijui kwanini hizi zimetengeneza taswira
nyingine kwa mashabiki,” alisema.
Ommy alisisitiza kuwa yeye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
Ex wa rafiki yake, na kuwa yeye na Wema walikuwa wakifahamiana hata
kabla ya Wema kuanza mahusia ya kimapenzi na Diamond. Hivyo kuacha kwao
haiwezi kumpelekea yeye awe mbali nao kwani hayo ni mambo yao binafsi.
Japokuwa Ommy anaamni kuwa kwenye pitapita za kimaisha inawezekana
mtu akawa na mahusiano ya kimapenzui na Ex wa rafiki yake, kwani hicho
kitu kinawezekana.
“Ku-date na Ex wa rafiki yangu, kwa mimi hapana lakini kuhusu maswala
ya mapenzi lolote linaweza kutokea kwasababu umesha sema Ex kwahiyo it
means hawapo kwenye mahusiono tena kwahiyo inaweza ikatokea huko mbele
mbele maisha yameendelea watu wakaja kukutana , kwa huyo vitu hivyo
vinawezekana” Dimpoz alieleza.
Picha za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo
na kuzua maswali mengi kwa mashabiki, kutokana na ukaribu aliyonao Ommy
Dimpoz na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema, Nasib abdul ‘Diamond’.
Facebook Blogger Plugin by AllyTz
Post a Comment